• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Complaints |
    • Gms |
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO
SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
    • Majukumu ya msingi
  • Utawala
    • Idara
      • Human Resources and Administration
      • Health and Sanitation
      • Finance
      • Planning and Commercial
    • Vitengo
      • Maintenance Service
      • Internal Audit
      • Procurement Management
      • Information and Communication Technologies
      • Legal Services
      • Security
  • Kituo cha habari
    • Habari
    • Matangazo
    • Maktaba ya picha
    • Press-Releases
    • Video
  • Marketing
    • Products and Services
    • Marketing Price
  • Miradi na Fursa za uwekezaji
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Manunuzi
    • Zabuni
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Journals/Newsletter
    • Reports
    • Hotuba
  • Huduma mtandao
    • Revenue Collection(TAUSI)
    • GISP Portal
    • Employees Self Service Portal
    • E - Mrejesho
    • E - Board
    • E - Mikutano

SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO, SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI JESHI LA POLISI WAKUTANA KUJADILI MIKAKATI YA ULINZI SOKO LA KARIAKOO.

Posted on: January 9th, 2026

SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO, SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI JESHI LA POLISI WAKUTANA KUJADILI MIKAKATI YA ULINZI SOKO LA KARIAKOO.

Shirika la Masoko ya Kariakoo limefanya kikao maalum na uongozi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi ambalo linatoa huduma za ulinzi katika soko la Kariakoo, kikao ambacho kimelenga kujadili namna bora ya kuimarisha ulinzi sokoni hapo.

Akiongea katika kikao hicho Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, CPA. Ashraph Abdulkarim amesema kufanyika kwa kikao hicho ni sehemu ya maandalizi ya ufunguzi wa soko hilo ambalo limekamilika kwa asilimia 99.

“Ni wajibu wetu kuona ni kwa namna gani kila mdau amejipanga kutoa huduma bora kwa wananchi na kufanya maboresho stahiki kabla ya ufunguzi wa soko, kwani litakapofunguliwa litajumuisha watu wengi ambao ulinzi wao pamoja na mali zao unatakiwa kuimarishwa na kuwa bora zaidi” ameongeza CPA. Abdulkarim.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi amesema shirika hilo litaendelea kushirikiana na Shirika la Masoko ya Kariakoo ili kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wa soko la Kariakoo wanapata huduma bora kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.

Aidha, amelishukuru Shirika la Masoko ya Kariakoo kwa kuwapatia mafunzo ya huduma bora kwa mteja kwa askari wa shirika hilo la Polisi na kuongeza kuwa mafunzo hayo yameongeza chachu ya utendaji kazi na uwajibikaji wa askari wake.

Matangazo

  • Taarifa kwa Umma January 31, 2025
  • Taarifa kwa Umma January 29, 2025
  • Usajili wa wafanyabiashara November 14, 2023
  • Tangazo la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 August 15, 2024
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO, SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI JESHI LA POLISI WAKUTANA KUJADILI MIKAKATI YA ULINZI SOKO LA KARIAKOO.

    January 09, 2026
  • WATUMISHI WA WASHIRIKA LA MASOKO WAJENGEWA UWEZO MATUMIZI YA E-MREJESHO.

    January 08, 2026
  • SOKO LA KARIAKOO LATENGA VYUMBA MAALUM VYAA KUNYONYESHA KWA WAKINA MAMA.

    December 30, 2025
  • UKARABATI NA UJENZI WA SOKO LA KARIAKOO WAFIKIA ASILIMIA 99, TAYARI KWA KUFUNGULIWA.

    December 24, 2025
  • Angalia zote

Video

Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • TAMISEMI
  • eGovernment Authority
  • Employees Self Service Portal

Viunganishi Linganifu

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

Visitors Counter

www.freevisitorcounters.com

    • Maswali ya Mara kwa Mara
    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.