SOKO LA KARIAKOO LATENGA VYUMBA MAALUM VYAA KUNYONYESHA KWA WAKINA MAMA.
Shirika la Masoko ya Kariakoo limetenga vyumba maalum vya kunyonyeshea watoto katika soko la Kariakoo, vyumba hivyo ni maalum kwa wakina mama ambao ni wafanyabiashara wa soko hilo kunyonyeshea watoto wao katika mazingira rafiki na yenye staha.
Kutengwa kwa vyumba hivyo ni utekelezaji wa maagizo ya serikali ambayo yanalenga kuwaondolea usumbufu wakina mama wanaonyonyesha na pia kuboresha afya ya watoto wao jambo ambalo litaondoa changamoto za udumavu kwa watoto kwa kutambua kuwa kuwa maziwa ya mama kwa watoto ni hitaji la msingi.
Akifafanua kuhusu kutenga vyumba hivyo, Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, CPA. Asharaph Abdulkarim amesema uongozi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo kwa kutambua umuhimu wa afya ya mtoto na ustawi wa wafanyabishara wake limeamua kutenga vyumba hivyo ili kumuondolea mama usumbufu na gharama za kwenda nyumbani au maeneo mengine kwa ajili ya kumnyonyesha mtoto wake.
“Kwa niaba ya menejiment naendelea kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwajali wafanyabiashara ambao amewajengea miundombinu ya kisasa kabisa hapa Kariakoo ambapo pamoja na maeneo ya biashara yapo pia maeneo ya huduma za kijamii ambayo yanamgusa mwananchi moja kwa moja” ameongeza CPA. Abdulkarim.
CPA. Abdulkarim amesema kuwa pamoja na vyumba vya kunyonyeshea watoto kwa wakina mama, serikali imejenga miundombinu kwa ajili ya watu wenye mahitaji maalum kwa kutambua kuwa soko hilo linahudumia wananchi wenye mahitaji mchanganyiko kutoka maeneo mbalimbali.
Ujenzi na ukarabati wa soko hilo umegharimu takribani Bilioni 28 ambapo ujenzi na ukarabati huo umekamilika kwa asilimia 99 ambapo tayari wafanyabisahara 1520 wa zamani wameshapangiwa maeneo ya kufanyia biashara, huku wafanyabiashara wapya 351 wakipangiwa maeneo kufuatia kuomba maeneo hayo kupitia mfumo wa TAUSI.
General Manager, Kariakoo Markets Corporation, Nyamwezi/Tandamti Street,
Anuani ya posta: P. O. Box 15789 Dar es Salaam, Tanzania
Simu: +255 22 2180678
Simu ya kiganjani:
Baruapepe za Watumishi: info@kariakoomarket.co.tz
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.