TAMISEMI, SHIRIKA LA MASOKO YA KARIAKOO WAANZA UTEKELEZAJI WA MAAGIZO YA RAIS WAKATI WA UFUNGUZI WA SOKO KUU LA KARIAKOO
Uongozi wa Shirika la Masoko ya Kariakoo umekutana na viongozi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa lengo la kukagua na kujadiliana mahitaji ya eneo la kulelea watoto ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Februari 8, 2026 wakati wa ufunguzi wa Soko Kuu la Kariakoo.
Baada ya kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya kujenga miundombinu ya kisasa yenye kukidhi viwango vya kimataifa, viongozi hao wamekubaliana kuwa wataalam wataandaa taarifa ya kina ambayo itawezesha kutekeleza agizo hilo la Mhe. Rais kwa haraka na kwa ubora unaotakiwa.
Viongozi hao wa TAMISEMI wameambatana na viongozi na wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, pamoja na wataalam Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
Copyright ©2024 Shirika la Masoko ya Kariakoo . All rights reserved.